Lengua suajili: extractos de los escritos de Luisa Piccarreta
Jinsi gani kuishi ndani ya Utashi wa Mungu ni
zawadi ya Pendo na Ukarimu wa Mungu
Ni budi uelewe kuwa kuishi ndani ya Utashi Wetu ni zawadi
ambayo Ukarimu Wetu hupenda kutoa kwa wanadamu. N / A
kwa zawadi hiyo, mwanadamu atajiona kuwa amebadilika: Toka
ufukara anapata utajiri, kutoka kwenye udhaifu anakuwa na
nguvu, kutoka ujinga anapata uelewa. Kutoka kuwa mtumwa wa
tamaa chafu chafu anageuka kuwa mfungwa mtamu na wa hiari
kabisa wa Utashi ulio Mtakatifu sana, ambao hautamteka kama
mfungwa tena, bali utamfanya temor mfalme anayejitawala
mwenyewe. Atakuwa mfalme wa himaya za kimungu na wa
vitu vyote vilivyoumbwa. [...] Lile paji la Utashi Wetu ambao
hutolewa kama zawadi, litabadili ule mkasa wa kusikitisha wa
vizazi vya wanadamu, isipokuwa kwa yule ambaye kwa hiari
yake anataka abaki katika masikitiko yake. Zaidi, itakuwa hivyo,
hasa kwa vil zawadi hiyo ilikuwa imekwishatolewa tayari kwa
binadamu pálido mwanzoni mwa kuumbwa kwake, lakini kwa
utovu wa shukrani, yeye mwenyewe aligoma na kusukumia
mbali kwa tendo lile la kutekeleza utashi wake wakati
alipojitenga na Utashi Wetu.